KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO MSAMBWENI.


 

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho ameendeleza kampeni ya kumpigia debe mgombea wa chama cha ODM Omar Boga ,kurithi nafasi ya ubunge wa Msambweni iliyowachwa wazi na aliyekuwa mbunge Suleiman Dori.

Joho ambaye pia ni naibu kinara wa chama hicho, amesema kuwa Boga ndiye chaguo la serikali kufuatia ushirikiano wa kinara wa ODM Raila Odinga na rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza katika wadi ya kinondo mapema leo, Joho amemtaja Boga kama kiongozi a,liyependezwa na serikali kuyatatua matatizo ya watu wa Msambweni.

Hata hivyo, gavana wa Kwale Salim Mvurya anayemuunga mkono mgombea huru Feisal , amempinga vikali Joho akisema hakuna mgombea anayependekezwa na rais Uhuru Kenyatta.

Kwa upande wake Feisal amewataka wakaazi wa Msambweni kumchagua kiongozi binafsi ,badala ya kuegemea upande wa chama.