Kampeni yamitandaoni kuokoa kituo cha afya cha Kongowea.


Mashirika ya kijamii sasa yanataka serikali ya kaunti ya Mombasa kuchukua hatua baada ya kubainika kuwa kituo cha afya cha Kongowea kimekuwa kikitumika kama sehemu ya kuegesha magari yanayoelekea soko la Kongowea.

Mashirika hayo yakiongozwa na shirika la Kwacha Afrika yameanzisha kampeni mitandaoni kutaka kituo hicho kushughulikiwa mara moja ikiwemo kuondolewa malori kama maegesho huku ikibainika kuwa pia inatumika kama sehemu ya kuuza bidhaa za sokoni.