Kampeni kufufua utalii yaanzishwa Kilifi.


Wadau wa sekta ya utalii kule watamu kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na wasanii mbali mbali wameanzisha kampeni kabambe ya kufufua utalii ambao umesambaratika kabisa katika siku za hivi karibuni.

Wadau hao wanadai kuwa lengo la hatua hiyo ni kufufua uchumi ambao umesambaratika hata zaidi hivi sasa.

Kulingana na Nicola Traldi, amaye ni mkurugenzi mkuu wa Solo Grano ambayo ni kampuni ya kupanga ghafula mbali mbali amesema wanapanga kongamano kubwa kule Watamu litakalo waleta Pamoja wadau mbali mbali wa sekta ya utalii.

Ni Kongamano ambalo linatarajiwa kufanyika mnamo mwexzi machi mwaka 2021.

Hatua hii inajiri juma moja baada ya ghafula kama hiyo kuandaliwa na wasanii katika hoteli moja eneo hilo.