Kamati ya BBI yatetea mapendekezo yao


Kamati maalum iliyoshughulikia ripoti ya BBI imetetea mapendekezo yaliyoangaziwa katika ripoti hiyo.

Kupitia naibu mwenyekiti Adams Oloo, kamati hiyo imesema kuwa yaliyoangaziwa katika maopendkeekzo hayo ni masuala yaliyowasilishwa katika vikao vyao kutoka kaunti mbalimbali nchini, yakiwa na manufaa kwa taifa.

Naye Mwanachama wa kamati ya BBI Wakili Tom Macharia ametetea mfumo wa uongozi unaopendekezwa kuu ikiwa uchaguzi huru na wa haki kupitia sura mpya ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Ametaja pendelezo la kuwa na majukumu wazi kwa naibu gavana katika kaunti nchini kando na kuundwa kwa afisi ya kiongozi wa upinzani nchini.

Naye mwenzake Paddy Onyango ameshabikia mabadiliko yanayopendekezwa kuhusiana na tume ya IEBC