Kamati ya afya katika bunge la kaunti ya Mombasa kuzuru daraja la Liwatoni.


Kamati ya afya katika bunge la kaunti ya Mombasa limetembelea daraja la Liwatoni katika juhudi za kutathmini kuhusu msongamano wa abiria kwenye daraja hilo.
Hii ni baada ya hoja kuhusu msongamano kwenye daraja hilo ambao huenda ukaleta athari ya maambukizi ya virusi vya corona kuwasilishwa na mwakilishi wa wadi ya Bofu Ahmed Salama.

Salama alitaka kujua je hakuna hatari ya maambukizi kwa kuwa abiria wote wameagizwa kutumia daraja hilo nyakati za asubuhi na jioni.

Pia kujua aliyetoa agizo hilo bila kutathmini kuhusu msongamano.

Kamati hiyo inayoongozwa na Kibwana Swaleh ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Miritini inatarajiwa kuwasilisha ripoti kamili kuhusu tatizo hilo mbele ya bunge wiki ijayo.