jowie huru baada ya siku 533


Joseph Irungu maarufu kama ‘Jowie’ ameachiliwa huru kutoka kwa gereza la Kamiti.

Hii ni baada ya kulipa dhamana ya Shilingi milioni 2, siku 533 baada ya kukamatwa kuhusiana na mauaji ya Monica Kimani hapa Nairobi.

Jaji wa mahakama kuu James Wakiaga alimuachilia Jowie kwa dhamana ya shilingi milioni 2 tarehe 13 mwezi uliopita baada ya juhudi zake za muda mrefu kushinikiza hilo kugonga mwamba.

Aliagizwa kukabidhi stakabadhi zake za usafiri sawa na kuripoti kwa afisi ya chifu mara moja kila mwezi huku akizuiwa kuzungumzia kesi hiyo hadharani.