Janga la Corona laathiri wasichana Taita Taveta


Imebainika kuwa mtoto wa kike katika jamii ameathirika zaidi kutokana na janga la virusi vya corona hasa baada ya shule kufungwa.

Baadhi ya wazazi wamesema kuwa changamoto ya kukosa sodo iliwafanya watoto wa kike kujiingiza katika ngono ya mapema na hivyo kusababisha mimba zamapema miongoni mwa changamoto zingine.

Naye mwenyekiti wa shirika la sauti ya wanawake Mwangea Macrina Mwamburi amesema kuwa katika kipindi hiki shirika hilo limerekodi asilimia kubwa ya dhulma za kijinsia dhidi ya mtoto wa kike.

Macrina ameongeza kuwa watoto wengi wa kike wamekumbana na changamoto za kunajisiwa, ndoa za mapema  na kufanywa kama walezi wa wenzao wadogo huku wengine wakipewa jukumu la kutafutia familia mapato.