Idara ya utawala wa mikoa Kilifi ,yaonya wazazi dhidi yakukosa kuwapeleka watoto shuleni.


Idara ya utawala wa mikoa kule kaunti ya Kilifi sasa wanawataka wazazi katika eneo hilo kukoma kabisa kuwaweka Watoto wao nyumbani na badala yake kuwasajili katika mashule.

Ni baada ya kubainika kuwa asilimia kubwa ya wazazi kanda hiyo hutumia kisingizio cha kukosa karo na kuwaacha Watoto wao nyumbani badala ya kuwafikisha shuleni.

Taarifa ya afisi hizo za utawala zinajiri kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta kwamba kila mwanafunzi ajiunge na shule humu nchini.

Kulingana na idara hiyo ya utawala yeyote atakaye patikana hajapeleka Watoto wake shuleni basi serikali haitakuwa na budi ila kumuandama kisheria.

Chifu wa eneo la fumbini Dickson Kitole asema kuwa msako dhidi ya wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao shule pamoja na watoto wao ungalipo.

Kulingana na kitole kuna idadi kubwa ya watoto kaunti ya kilifi ambao bado wanarandaranda mitaani bila kuhudhduria masomo.