IDARA YA USALAMA NA MIKAKATI YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA CORONA MPAKANI KENYA NA TANZANIA.


Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeweka mikakati kabambe ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona katika mpaka wa Kenya na Taifa jirani la Tanzania.

Kamishena wa kaunti hiyo Joseph Kanyiri amesema kuwa ,ni sharti raia wanaoingia Kenya kupitia mpaka wa Lungalunga wachunguzwe na kupimwa virusi hivyo vya corona.

Wakati uo huo, kamishena huyo amewaonya vikali wakaazi hao ,dhidi ya kutumia njia za mkato katika maeneo ya mpakani kwamba watashtakiwa