Idara ya usalama kuwasaka wasiovaa barakoa Lamu.


Idara ya usalama katika kaunti ya Lamu imeanzisha msako mkali wa kuwasaka wakaazi ambao watapatikana bila kuvaa barakoa kwamba watakabiliwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema ni jukumu la kila mwananchi kuvaa barakao ili kujiziba mdomo kama njia moja wapo ya kudhibiti  maambukizi ya virusi vya korona.

Oparesheni hiyo imeanzishwa baada ya wakaazi wengi Lamu kuonekana wakitoka nje ya nyumba zao ,sawa na kuwa barabarani bila  kuwa na mabarakoa jambo linalohatarisha afya yao.

Kadhalka Macharia amewasihi wakaazi kuendelea kuzingatia maagizo yaliyotolewa na serikali kuu ili kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo ikiwemo kuosha mikono yao mara kwa mara ,kutosalimiana kwa mikono sawa na kuepukana mikusanyiko.