HURIA-MDAHALO WA WAGOMBEA WA KITI CHA UBUNGE WA MSAMBWENI.


Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA limeandaa mdahalo wa wagombea wa kiti cha ubunge wa Msambweni ,katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa eneo hilo.

Kulingana na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Yusuf Lule, mdahalo huo umewajumuisha wagombea wanne, kati ya saba wanaoshiriki katika kinyanga’nyiro hicho.

Vile vile Lule ameelezea kutofurahishwa na hatua ya baadhi ya viongozi kupuuza mdahalo huo ,unaolenga kukabiliana na siasa zisizofaa.

Mkurugenzi huyo amewataka wakaazi wa Msambweni kufanya uamuzi wao kwa busara ,katika uchaguzi huo wa tarehe 15 Disemba.

Wagombea Sheikh Abdulrahman wa Wiper, Hassan Mwakulonda wa Party of Economic Democrasy, Khamis Mwakaonje wa United Green Movement na mgombea huru Mansur Kumaka, wameshiriki mdahalo huo.