HUDUMA NAMBA HAZIJACHUKULIWA,TANA RIVER.


Takribani kadi 800 za Huduma Namba bado ,hazijachukuliwa na wenyewe katika afisi ya Kamishna wa kaunti mjini Hola kaunti ya Tana River,na hii ni miezi miwili baada ya kadi hizo za awamu ya kwanza kutolewa na serikali.

Kulingana na Msaidizi wa Kamishna wa kaunti, Geoffrey Mwachofi, wamepokea kadi 1,058 mnamo mwezi disemba ,lakini zile ambazo zimechukuliwa na wenyewe kufikia sasa ni 268 ,hivyo kuwahimiza wakaazi kuhakikisha wamechukua kadi hizo.

Aidha, anasema wanafanya mpango kuhakikisha wanazipeleka kwa maafisi za manaibu wa kamishna huko Bura na Garsen, ili wakaazi wa eneo hilo ,waweze kuzipata kwa ukaribu badala ya wao kusafiri hadi mjini Hola.