Hoteli ya kitalii Voi yafungwa.


Hoteli ya kitalii ya Voi Wildlife ambapo mtalii wa asili ya Ufaransa aliyepatikana na virusi vya Corona alikaa kwa siku moja hatimaye imefungwa.
Kulingana na meneja wa hoteli hiyo Agostine Mwanake anasema wamechukua hatua hiyo kama njia ya kuwakinga wafanyikazi wengine waliotangamana na mtalii huyo kuambukizana virusi hivyo.

Mwanamke anasema jumla ya wafanyikazi saba walitangamana na mtalii huyo huku sasa mfanyikazi mmoja akibakia katika chumba maalum katika hoteli hiyo kwa kuwa anatoka sehemu za bara.

Aidha wafanyikazi wengine wawili wako katika mtaa wa Mwakingali na Sophia viungani mwa mji wa Voi wakijiangalia hali yao nao wengine wakirudi kaunti za Mombasa na Kilifi.

Mwanake ambaye pia ni mwenyekiti wa hoteli za kitalii kaunti ya Taita Taveta amekiri kwamba wageni wengi wamesitisha safari zao huku hoteli zikiendelea kukadiria hasara.