Hospitali ya Getrudes yasalimu amri


Hospitali ya Gertrudes imekubali kuachilia mwili wa mtoto Brian Kimani kwa mazishi baada ya kufanya mkutano na familia ya marehemu kujadili jinsi ya kulipa deni ambalo wanadaiwa na hospitali hiyo.

Afisa mkuu wa fedha hospitalini humo Barak Kerich,anasema wamekubaliana na familia hiyo ni lini wanaweza kuchukua mwili wa Brian na kwamba hospitali hiyo haitazungumzia lolote kuhusu deni hilo.

Stephen Njoroge babake marehemu anasema usimamizi wa hospitali umekubali kufutilia mbali deni la shilingi milioni 1.5 kati ya shilingi milioni 17.9 wanalodaiwa na hivyo wamesalia na deni la shilingi milioni 11.89..

Njoroge anawarai wakenya kumsaidia kulipa deni hilo akisema hajakuwa kazini kwa muda wa miaka miwili tangu kuugua kwa mwanawe na hadi kufariki kwake mwezi jana.

Brian Kimani mwenye umri wa miaka 13 alifariki baada ya kuugua saratani.