hatuna pesa zaidi mnazotaka- Uhuru


Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa serikali kwa sasa haina pesa za kuangazia uhaba wa bajeti ya idara ya mahakama.

Rais Kenyatta amewataka maafisa wa idara hiyo na maafisa wengine serikalini kuwa na mazoea ya kupunguza gharama ya matumizi kw akutumia kidogo wanachopokea.

Kauli yake inatokana na lalama kutoka kwa jaji mkuu David Maraga anayelalamikia kupunguzwa kwa bajeti ya idara ya mahakama.

Anadai kuwa kuna mrundiko wa kesi katika idara hiyo hali ambayo imechangiwa na ukosefu wa pesa za kutosha.