Hali ya ukavu kushuhudiwa hadi Oktoba


Idara ya utabiri wa hali ya anga inasema kuwa maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kushuhudia vipindi vya jua na hali ya ukavu mwezi huu wa Septemba, isipokuwa maeneo yaliyo magharibi ya Kenya, Ziwa Viktoria na maeneo yaliyo katikati ya bonde la ufa.

Taarifa kutoka idara hiyo inasema kuwa  Maeneo yaliyo katikati ya nchi yanatarajiwa kushuhudia baridi ya muda tu na mawingu katika mida ya asubuhi na mvua katika mida ya mchana, hasa katika siku za mwanzo wa mwezi wa mwezi huu wa  Septemba.

Hali ya jua na ukavu vinatarajiwa katika maeneo ya kaskazinimashariki, kusini mashariki na kaunti za Pwani.

Yakijiri hayo, maeneo mengi ya nchi huenda yakapokea mvua ya viwango vya chini ya wastani msimu wa Mvua za Vuli wa Oktoba-Novemba-Disemba.

Hali hii inatokana na hali ya viwango vya wastani vya joto baharini  katika maeneo ya magharibi ya bahari ya Hindi.