HAKUNA LIKIZO KWA WAHUDUMU WA AFYA


 
Madaktari na wahudumu wa afya katika kaunti ya Taita Taveta hawataruhusiwa tena kuenda kwa likizo ya masomo ya ziada (long term trainings).

 
Katika barua ilitiwa saini na kaimu afisa mkuu wa wizara ya afya katika kaunti hiyo Nestror Mwasaru, serikali ya kaunti imesimamisha utoaje wa likizo za masomo kwa wafanyikazi wa sekta ya afya japo haijawekwa bayana sababu ya hatua hiyo.
 
Awali gavana Granton Samboja alikuwa ametoa tahadhari kwa madaktari na wauguzi wanaozembea katika majuku yao na kusisitiza kuwa sharti idara hiyo iboreshwe zaidi kwa kuimarisha huduma haswa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi.
 
Samboja aidha anasema watahakikisha wahudumu wa afya hasa wanaoshuhulikia wagonjwa wa virusi vya Corona wataangaziwa vilivyo.