HADI KUFIKIA SASA WAHUDU WA AFYA 45 MOMBASA WAMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA


 

Serikali ya kaunti ya Mombasa imesema kwamba tangu kuibuka kwa janga la Corona, takriban wahudumu wa afya 1,250, wameweza kupimwa virusi vya hivyo ambapo jumla ya wahudumu 45 wameweza kupatikana na ugonjwa huo.

Waziri wa afya kaunti hii ya Mombasa Bi Hazel Koitaba ,amesema kwamba lengo la kuwapima wahudumu wa afya ni kuhakikisha wako salama na hasaa ikizingatiwa kwamba wao wako katika mstari wa Mbele kwenye zoezi hilo.

Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema kwamba jukumu la vita dhidi ya uogonjwa huo liko mikononi mwa wananchi kwa misingi kwamba serikali sawia na wahisani wamejitokeza ipasavyo kwa kununua vifaa hitajika.

Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani ,walipopokea msaada wa vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huo vilivyotolewa na benki ya Equity.