GAVANA WA TANA RIVER ASITISHA SAFARI ZOTE ZA MAGARI YA UMMA .


Gavana wa Tana River Dhadho Godhana apiga marufuku usafiri wa umma kaunti hiyo kwa muda wa siku 14 ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona eneo hilo.

Akiongea katika kituo kimoja cha radio mjini Hola, Godhana anasema usafiri wa matatu, mabasi, tuktuk, pikipiki na probox zimepigwa marufuku kwa muda wa siku 14 kuanzia leo na magari ya kibnafsi ndio yataruhusiwa kuingia mjini kaunti hiyo.

Aidha, magari hayo ya kibnafsi sharti yafanyiwe ukaguzi na maafisa wa afya katika vituo vyote vya kuingia kaunti katika eneo la Gamba, Hurara, Mororo na Bangale.

Hayo yanajiri huku watu wanne ikiwa wanazuiliwa katika taasisi ya matibabu ya KMTC mjini humo baada ya kukutana na mkazi mmoja kutoka kaunti hiyo ambaye ameingia nchini hivi majuzi na hakuzingatia kanuni zilizowekwa na serikali za kujitenga na umma