Gavana wa Mombasa awasuta wanaokosoa azma yake ya urais.


Gavana wa Mombasa Hassan Joho ameendeleza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake wanaosema kuwa hawezi kushinda kiti cha urais.

Joho amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kuwa baadhi ya viongozi hata kutoka Mombasa wanamrushia makombora na kumkebehi kuwa hawezi kuwa rais bila kutoa sababu za maana.

Gavana huyo akiwaonya wakosoaji wake kujitayarisha kwani anaendelea kupasha misuli moto kuhakikisha yuko katika kinyang’anyiro hicho cha mwaka 2022.

Akizungumza mjini Mombasa Joho amesema kuwa yuko tayari kupambana katika kuwania urais na wote watakaokuwa debeni.

 

Ni jambo ambalo mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir na mwenzake wa Likoni Mishi Mboko wamesema kuwa kila eneo la nchi linaweza kuzalisha kiongozi latina ngazi za kitaifa.