Gavana wa Lamu awasisitiza wakaazi kuvaa barakoa .


Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Twaha amewahimiza wakaazi wa Lamu kuendelea kuvaa maski ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya korona.

Katika kikao wa wanadishi wa habari Gavana Twaha amewasihi wakaazi kutokuwa na nadharia kwamba uvaaji wa maski ni usumbufu au inasababisha magonjwa akisema ni kinga yao wenyewe.

Amewataka wakaazi kustahili na kuendelea kufata maagizo yaliyotolewa na serikali kuu ili kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo hadi pale virusi hivyo vitakapofika kikomo.

Swala la uvaaji wa maski kwa wakaazi wengi haswa katika maeneo ya visiwani Lamh limekuwa swala sugu huku wengi wakiamini kwamba Lamu iko salama hakuna virusi vya korona.