Gavana wa kaunti ya Kwale azindua zoezi la kukusanya sahihi za BBI Ukunda.


Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya ameunga mkono pendekezo la ripoti ya BBI, hususan kipengee cha kubuni maeneo bunge matatu katika kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa kutia saini ripoti ya BBI huko Ukunda, Mvurya amesema hatua hiyo itaongeza mgao wa fedha wa hazina ya CDF katika kaunti hiyo, hivyo wa Kwale watafaidika kimaendeleo.