GAVANA KUBORESHA SEKTA YA UTALII


Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Yasin Twaha ametakiwa kuboresha sekta ya utalii katika kaunti ya Lamu kwani ndio sekta kuu inayotegemwa na asilimia kubwa ya wakaazi wa Lamu.

Kulingana na mmiliki wa Hoteli Ali Buno Lamu kiwanda cha peke ni utalii ambapo wenye mahoteli,mama mboga,wenye  punda,wafugaji,wavuvi wote upata fedha kutoka kwa watalii pindi wanapozuru eneo hilo.

Buno amesema iwapo watalii watakosa kuzuru eneo hilo basi maswala ya uhalifu na janga la umaskini litazidi kukithiri katika kaunti hiyo kutokana na makali ya maisha.