GAVANA JOHO APATIKANA NA HATIA YA KUKIUKA AGIZO LA MAHAKAMA


Mahakama ya Mombasa imempata na hatia gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kwa kukiuka agizo la mahakama na kuvunja ukuta uliozingira shamba lililo na utata kule Changamwe Mombasa.

Akitoa uamuzi huo Jaji Silas Munyao amesema kwamba Gavana Joho ushirikiano na mwakilishi wa wodi katika eno la Changamwe Bernard Ogutu walipuuzilia mbali agizo la mahakama iliositisha shughli zozote za ubomoaji wa jengo linalomilikiwa na mfanyibiashara Ashok Doshi.

Kwenye kisa hicho Joho alidai kuwa mfanyibiashara huyo alikuwa amenyakua sehemu ya ardhi ya shule ya sekondari ya Changamwe na hivyo kuapa kwamba shamba hilo litaregeshwa mikononi mwa shule hio na hivyo kuvunja ukuta huo kinyume na agizo la mahakama.

Gavana Joho sasa anatarajiwa kuandamana mahakamani na mwakilishi wa wodi Bernard Ogutu kupewa hukumu yao (civil sentence).