GAVANA ATAKIWA KUTATUA TATIZO LA MOTO


Mshauri wa afisi ya gavana wa kaunti ya Lamu Shekue Kahale amemtaka gavana wa Lamu Fahim Twaha kutatua tatizo la ukosefu wa nguvu za umeme ambalo limekuwa swala sugu katika kaunti hiyo.

Kulingana na Kahale kwa zaidi ya muda wa miezi mitatu sasa umeme kaunti ya Lamu ikiwemo maneo ya Visiwani umekuwa ukipotea mara kwa mara hali inayopelekea wavuvi kukadiria hasara ya samaki wao kuharibika.

Amesema wakaazi wa Lamu wanalipa ushuru kama wakaazi wengine akishangaa ni vipi moto umekuwa ukipota kwa muda  pasipo kuwa na suluhisho la kudumu.