FERRY LIKONI MOMBASA KUHUDUMU HADI SAA KUMI NA MBILI JIONI


Mshirikishi wa serikali katika ukanda wa pwani John Elungata amesema kwamba huduma zote za ferry katika kivuko cha Likoni mjini Mombasa zitasitishwa kuanzia saa saa kumi na mbili jioni kuanzia siku ya Ijumaa hadi saa kumi na moja asubuhi.

Hii nikufuatia agizo lililotolewa na rais Uhuru Kenyatta ya kupiga marufuku wanachi dhidi ya kutembea kati ya saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri.

Akizungumza katika kivuko cha likoni Ferry Elungata aidha amesema kwamba kwa kipindi cha abiria wengi, ferry tatu zitakuwa zinabeba abiria huku ferry moja ikitengewa magariyatakaayokuwa yaanavukishwa kutoka ngambo moja hadi nyingine.

Aidha kamishna huyo ameshikilia kwamba hakuna yeyote atakaye ruhusiwa kuabiri ferry bila kuvaa barakoa au kitambaa cha kuzuia mdomo na pua.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la Kenya Ferry Bakari Goa amesema kwamba wanaapanga kuweka alama kwenye ferry hizo kuonyesha sehemu ambazo watu watastahili kusimama ilikutoa nafasi ya abiria kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa kila abiria.