Familia Chonyi, yanyimwa haki ya kuzika mwili wa mpendwa wao.


Familia moja katika eneo la Ziani, Chonyi kaunti ya Kilifi inataka usaidizi wa kuruhusiwa kuzika mwili wa mpendwa wao baada ya kuzuiliwa kufanya hivyo na mahakama.

Mazishi ya marehemu Dorothy Mwamuye mwenye umri wa miaka 48 yalitibuka jumamosi baada ya jamaa aliyedaiwa kuwa mumewe kuwasilisha amari ya mahakama akitaka marehemu kutozikwa.