Demokrasia ya vyama inauawa nchini- Wetangula


Seneta wa Bungoma Moses Wetangula anadai kuwa kuna njama ya kuua demokrasia nchini kwa kupenyeza utawala wa kiimla katika vyama vya kisiasa nchini.

Hii ni kutokana na kauli kinzani na msimamo mikali kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa,matukio anayodai yamekithiri mwaka huu.

Katika mahojiano na runinga ya Citizen, Wetangula aidha amewashtumu walio na nia ya kuwazima kisiasa wanasiasa kutoka eneo la magharibi mwa nchi akisema hilo halitafaulu.