CHANGAMOTO ZA VIJANA KUKOSA VITAMBULISHO LICHA YA KUWASILISHA MAOMBI LAMU.


Imebainika kuwa vijana ambao walisajiliwa ili kupata vitambulisho miaka iliyopita katika kaunti ya Lamu ,wengi wao vijana hadi leo bado hawajapata vitambulisho hivyo.

Mbunge wa Lamu Mashariki Sharrif Athman amehuzunishwa kuona vijana wa Lamu wanakosa stakabadhi hiyo muhimu ,huku wengi wakisalia kuangahishwa na maafisa wa usalama .

Sharrif aidha amemtaka kamishna wa Lamu Irungu Macharia, kueka wazi kwa nini swala la vitambulisho kwa vijana wa Lamu linachukua muda mwingi ikilinganishwa na kaunti zengine.