Siasa za BBI zachukua kipau mbele wakati wa mazishi ya mamake aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana huko Ngao Tana Delta hii leo.
Siasa hizo zimewakutanisha Gavana Dhadho Godhana na mbunge wa Garsen, Ali Wario ambao wanaunga mkono BBI dhidi ya mwakilishi wa wanawake , Rehema Hassan, ambaye anapinga BBI na yuko mrengo wa kumpigia debe naibu rais, William Ruto.
Bi Hassan anasema kujihusisha kwake na Naibu wa Rais William Ruto kumumpelekea kupata msaada wa takribabi shilingi milioni 20 kupitia michango kwa wakazi wa Tana River ,na kwamba BBI inaondoa kiti cha mwakilishi wa wanawake ambacho ndio kiti pekee ambacho mwanamke anaweza kuchaguliwa kwa uongozi Tana River.
Ni kauli ambayo imepingwa vikali na Governor Godhana na mbunge Ali Wario ,wanaosema kaunti hiyo haitanawiri kimaendeleo kupitia fedha za michango, bali kupitia ongezeko la mgao kutoka kwa serikali kuu wa asilimia 35.
Godhana anadai sababu kuu ya mwakilishi huyo wa wanawake kupinga BBI ni kwamba ,inaondoa kipendee cha mwakilishi wa wanawake na kusema kuondolewa kwa nyadhifa hio ,hakujazuia wanawake kupigania nyadhifa nyengine.
Aidha, Godhana anahoji kwamba mchakato wa magavana Hassan Joho na Amason Kingi wa kuwa na chama cha kipwani ,ni mojawapo ya azma ya wapwani kuwa na nguvu ya kupigania nyadhifa za juu serikalini ,na kwamba Raila Odinga atakuwepo kwa debe kupigania urais mwaka wa 2022.