Bunge la uasin Gishu larejelea vikao


Bunge la kaunti ya Uasin gishu litaendelea kuandaa vikao vya muda mfupi ili kutekeleza shughuli mbalimbali huku masharti yote yaliyowekwa na wizara ya afya yakiwa yamezingatiwa vilivyo ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

Spika wa bunge hilo David Kiplagat amesema kwamba idadi ndogo ya wawakilishi wa wadi watakua wanaingia kwenye bunge hilo ili waweze kuzingatia sheria ya kukaa umbali wa mita moja wanapofanya shughuli mbalimbali bungeni.

Akizungumza kule Eldoret, Kiplagat amedokeza kwamba bunge hilo limekua likiandaa vikao mara moja kwa kila wiki ili kujadili masuala mbalimbali muhimu kwa kaunti hiyo.