BUNGE LA TANA RIVER LASHUTUMIWA KWA KUKOSA KUHUSISHA UMMA KABLA YA KUPITISHA RIPOTI YA BBI.


Bunge la kaunti ya Tana River lashtumiwa vikali kwa kupitisha mswaada wa kubadilisha katiba maarufu BBI bila kuhusisha umma, licha ya kuweka tangazo katika gazeti kwamba lingefanya vikao vya umma hapo kesho.

Ni hatua ambayo imepelekea baadhi ya wakazi kutishia kwenda mahakamani ,na tayari aliyekuwa mbunge wa Garsen, Danson Mungatana, amethibitisha kwamba kunao wakazi ambao wanataka wawasilishe kesi mahakamani kwa niaba yao ,dhidi ya kile wanasema ni bunge la kaunti kutofuata sheria.

Baadhi ya wanaharakati ambao wameongea na kituo hiki ,wamekashifu hatua hiyo na kusema bunge lingeandaa vikao vya umma, ili wananchi watoe maoni yao hata kama hawana uwezo wa kubadili chochote ,katika mswaada huo wa sheria.

Mwenyekiti wa kamati ya huduma ya umma na utawala katika bunge la kaunti, Mohammed Buya,ambaye mswaada huo wa shera umekuwa katika kamati yake ,hakuweza kutoa sababu maalum ya bunge kupitisha BBI ,bila kabla kufanyika kwa vikao vya umma.