Bunge la Kaunti ya Lamu lapitisha BBI.


Bunge la kaunti ya Lamu hatimaye limekuwa miongoni mwa mabunge mengine humu nchini kupitisha mswada wa BBI mapema leo katika makao makuu ya bunge eneo la Mokowe kaunti ya Lamu.

Wawakilishi wadi wote 18 miongoni mwao wabunge wateule wanane kwa kauli moja wote wameunga mkono ripoti ya BBI kabla ya kupitishwa mwendo wa saa tano kamili na Spika wa bunge Abdul Kassim Ahmed.

Aidha Mwakilishi wadi ya Shella Mbarak Azhar ametoa wito kwa wabunge wa kitaifa kuona kwamba baadhi ya vipengee ambavyo vinakandamiza wakaazi wa Lamu waweze kuvijadili katika bunge la kitaifa.