Biashara ya Mitumba marufuku Kwale.


Katika juhudi za kuendelea kudhibiti virusi vya corona katika kaunti ya Kwale , serikali ya kaunti hiyo imepiga marufuku uuzaji wa nguo za mitumba.

Pia kaunti hiyo imepiga marufuku masoko ya wazi ya kila wiki maarufu kama chete kama njia ya kudhibiti virusi hivyo.

Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya pia imetangaza kufungwa kwa soko la Ibiza katika eneo la Ukunda.

Wafanyibiashara hao aidha watahamishwa hadi uwanja wa Showground ili kuweza kutekeleza agizo la kuwa umbali mita moja.

Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema kuwa wataendelea kutekeleza maagizo yote ili kudhibiti virusi vya corona.

Haya yanajiri baada ya kaunti ya Kwale kutangazwa kuwa miongoni kwa kaunti zilizohatarini zaidi kupata na kusambaza virusi vya corona.