BBI yapingwa vikali Taita Taveta.


Wanachama wa chama cha United Green party movement kaunti ya Taita Taveta, wamesema kwamba watahakikisha mchakato wa BBI hautafanikiwa kaunti hiyo.

Wakiongozwa na Anna Nyambu wanasema mchakato wa bbi haujazingatia matakwa ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta, ikiwemo suala la mapato ya Tsavo na hivyo hawataiunga mkono.