BARAZA LA WAZEE WABAJUNI MOMBASA LATAKA KUTAMBULIKA NA SERIKALI.


Baraza la wazee wa kabila la wabajuni sasa wanaitaka serikali kuu kutambua baraza hilo ili waweze kushirikishwa katika maamuzi ya kitaifa kama mabaraza mengine ya wazee nchini.

Baraza hilo aidha linahisi kubaguliwa katika serikali licha ya kuwa miongoni mwa mabaraza mengine ya wazee hapa nchini.

Mwanzilishi wa baraza hilo Omar Shariff amesema katika kabila 43 za hapa nchini kabila la jamii hiyo limo ndani lakini linakosa baraza la wazee jambo linalowafanya kuachwa nyuma katika maamuzi mengi.