BARAZA LA WAZEE LAMU LAWASUTA VIONGOZI WA KISIASA KUHUSIANA NA MSIMAMO WA BBI.


Baraza la wazee katika kaunti ya Lamu limewakosoa viongozi wa kisiasa wa kaunti hiyo kuhusuana na msimamo wao wa ripoti ya BBI.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Shariff Salim Kambaa ,wazee hao wamesema viongozi wa Lamu wanaunga mkono BBI pasi na kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya ripoti hiyo.

Kambaa amesema viongozi wanapaswa kuisoma na kuielewa vyema BBI ,na pia kupata ushauri kutoka kwa wananchi wao, hivyo haifai kuwaamulia wananchi moja kwa moja.