Baraza la magavana na seneti lajadili namna ya kuboresha sekta kilimo nchini


Baraza la magavana kwa ushirikiano na kamati ya bunge la senate kuhusu kilimo imenyoshea wizara ya Kilimo kidole cha lawama kwa madai ya kuchangia kudora kwa maswala ya kilimo, uvuvi na ufugaji wa mifugo nchini.

Haya wameyasema mjini Mombasa baada ya kufanya mkutano wa pamoja kujadili na pia kuangazia maswala yanayonuia kuboresha sekta ya kilimo uvuvi na ufugaji wa mifugi humu nchini.