Barabara yafungwa Mombasa.


Barabara ya Miritini – Mwache – Kipevu imefungwa kwa muda wa saa 48, ili kufanyia marekebisho sehemu ndogo ya barabara hiyo.

Katika taarifa mamlaka ya barabara kuu KENHA imesema kuwa sehemu hiyo itafanyiwa marekebisho kutokana na unyevu jambo ambalo limefanya sehemu hiyo kuonyesha dalili za kuporomoka.