BAADHI YA VIJANA WALIOPEWA VIBARUA NA SERIKALI WADAI HAWALIPWA


Baadhi ya vijana mjini Mombasa walioajiriwa na serikali kufanya kazi mitaani sasa wanadai kwamba baadhi yao wahajapokea mishahara yao na hivyo kutaka kujua mbini inayotumika kutoa malipo hayo.

Ni hatua ambayo imepelekea mbunge wa Nyali Mohamed Ali kuwataka wahusika kuingilia kati na kutatua changamoto zilizoko na hasaa baada ya kubainika kwamkba baadhi yao tayari wamepkea hela za wiki mbili.

Matamshi ya mbuge huyo pia yameungwa mkono na Nicholus Otieno mkaazi wa mikindani.

Hata hivyo baadhi ya wasimamizi wa mradi huo wamekiri kwamba ni kweli baadhi ya vijana hawajapokea malipo yao kutokana na mkanganyiko wa majina huku wengine wakidaiwa kujiandikisha kwa kutumia vitambulisho vya watu tofauti na hivyo kutakiwa kufanya marekebisho hayo kabla ya kulipwa mishahara yao.