Ardhi tata ya ADC Sabaki-KILIFI


Jumla ya wakaazi 10,000 kutoka eneo la Moi Sabaki kule Malindi sasa wanaitaka serikali kupitia tume ya kitaifa ya ardhi NLC kuwapa hati miliki za ardhi hiyo.

Ardhi hiyo ambayo inachokima cha Zaidi ya ekari 900 imesalia kuwa wazi bila shuhuli zozote jambo ambalo limesababisha wanyakuzi kuivamia na kuipora.

Kulingana na mzee wa Kijiji eneo hilo la Moi Safari Kadenge wakaazi wengi wa eneo hilo wamesalia maskwota licha ardhi hiyo kuwa yao tangu jadi.

Amesema licha ya kuwashirikisha viongozi eneo hilo hakuna la kujivunia hadi sasa.

Aidha Kadenge amesema kwa sasa wakazi hao wameingiwa na wasiwasi kutokana na baadhi ya mabwenyenye ambao wameanza kuvamia ardhi hiyo wakidai kuanzisha miradi ya serikali.

Kwa sasa Kadenge anaitaka tume ya ardhi kutuma maafisa wake katika ardhi hiyo ili mipango ya maskwota hao kusajiliwa na kupewa hati miliki ya ardhi yao ianze mara moja