AKINA MAMA NA LALAMA ZA KUKOSA AJIRA LICHA YA KUWA NA VYETI .


 

Akina mama katika kaunti ya Lamu wamelalamika kukosa kupewa nafasi za kazi ,licha ya wao kujitokeza wakati wa uchaguzi kupiga kura kwa ajili ya matarajio ya maendeleo na ajira.

Wakiongozwa na Sharrifa Abubakar amesema ,afisi nyingi za serikali ikiwemo serikali ya kaunti , akina mama wa Lamu walioajiriwa ni wachache mno,huku kwa uapnde wa nafasi za bandari wakikosa kuzingatiwa.

Shariffa aidha amesema akina mama wengi Lamu wamehitimu kuwa na vyeti vya taaluma mbalimbali, lakini serikali imekosa kuwapa nafasi za kazi ,huku nafasi zao zikipewa wanawake kutoka nje ya kaunti hiyo.