AKINA MAMA KUHUSU UTUMIZI WA MIHADARATI-TAITA TAVETA.


Changamoto imetolewa kwa idara ya usalama kushirikiana na wakaazi ,ili kumaliza tatizo la mihadarati katika mji wa Voi na viunga vyake.

Kulingana na shirika la akina mama la Sauti ya wanawake, wanasema ongezeko la utumizi wa mihadarati miongoni mwa vijana ,unazidi kila uchao.

Aidha wametoa wito kwa serikali ya kaunti ,kuharakisha ujenzi wa chumba cha kurekebisha uraibu wa mihadarati.