Afueni kwa wafanyibiashara Taveta.


Huenda wafanyibiashara kaunti ya Taita Taveta wakapata afueni ya makataa yaliyotolewa na serikali ya kaunti hiyo ya kuwataka kulipia leseni zao kabla ya tarehe 31 mei .

Hii ni Kufuatia hatua ya naibu mwenyekiti wa kamati ya fedha katika bunge la kaunti hiyo Joan Adino kuitaka serikali ya kaunti hiyo kueleza sababu ya wafanyibiashara wadogo kulazimishwa kulipia leseni za biashara zao kabla ya mwisho wa mwezi mei.

Adino ametamaushwa na agizo hilo akilitaja kuwa mzigo mzito kwa wafanyibiashara ambao tayari wameathiriwa mno na mikakati iliyowekwa kukabiliana na janga la corona huku ilazimu baadhi ya biashara zao kufungwa kwa mda usiyojulikana.

Akisimama katika hoja ya nidhamu bungeni humo Adino amemtaka waziri wa fedha na mipango ya serikali ya kaunti hiyo Andrew Kubo kutoa sababu za kuwalazimisha wafanyibiashara kulipia leseni zao wakati huu mgumu.