Afisa wa kijeshi aliyemuuwa mkewe na kisha kujiua kutopewa mazishi ya kiserikali .


Afisa wa Gsu aliyekuwa katika kitengo cha kulinda watu mashuhuri anayedaiwa kumpiga risasi mkewe ambaye ni afisa wa trafiki wiki jana jijini Nairobi kabla ya kujipiga risasi atazikwa nyumbani kwo huko Rong’e eneo bunge la Voi kaunti ya Taita Taveta.

Hata hivyo imebainika kwamba afisa huyo Hudson Wakise hatapewa mazishi ya kiserikali na badala yake familia yake italazimika kumzika kama mwananchi wa kawaida.

Mkewe Pauline Wakasa tayari alizikwa siku ya jumamosi juma lililopita katika kijiji cha Matsakha kaunti ya Kakamega.