ACHANI NA HAMASA KWA WANAWAKE KUHUSU VISA VYA DHULMA ZA KIJINSIA- KWALE.


Naibu Gavana wa Kwale Fatuma Achani ameanzisha mpango wa kuwahamasisha wanawake, kuhusu jinsi ya kuvikabili visa vya dhulma za kijinsia katika jamii.

Achani amesema kuwa hamasa hizo ,zinazotolewa kwa makundi ya wanawake zinalenga kuwaelimisha na kuwalinda dhidi ya visa hivyo.

Vile vile Achani amesema kuwa ,waathiriwa wakuu wa visa hivyo vya dhulma ni wanawake na watoto wadogo.