Abiria wajeruhiwa baada ya ajali Voi.


Abiria wanane wamejeruhiwa vibaya baada ya Matatu walimokua wakisafiria kuhusika katika ajali eneo la Show ground barabara ya Voi kuelekea Mwatate kaunti ya Taita Taveta.

Inaarifiwa ajali hiyo ilitokea baada ya Matatu walimokua wakisafiria kupasuka gurudumu la mbele na kusababisha kuoteza mwelekeo na kubingiria mara kadha.

Tayari abiria waliohusika katika ajali hiyo wamekimizwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kwa matibabu zaidi huku polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi.