Wito wa walimu kulipwa Taita Taveta.


Changamoto imetolewa kwa wabunge wa kaunti ya Taita Taveta kushirikiana ili kuishinikiza wizara ya elimu kuwalipa walimu wote wanaohudumu kwenye kaunti hiyo malipo ya kuhudumu katika mazingira magumu.

Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime anasema umoja wa wabunge wa kaunti hiyo ni nguzo muhimu katika kufanikisha hilo kwani waalimu wengi wanapitia wakati mgumu.